Fuga Kidigitali Zaidi

Tunza kumbukumbu zako, Wasiliana na Wataalamu, Pata Masoko Kiganjani mwako!

Fahamu Zaidi
pic

Watumiaji Walengwa wa Agripoa

Hapa wafugaji wanaweza kutumia mfumo huu kurahisisha zaidi kazi zao kwa kutunza kumbukumbu, kujua habari za masoko, kuunganishwa na wauzaji wa pembejeo za mifugo, kuunganishwa na watoaji wa mikopo, nk.
Mtu yeyote anayekutana na changamoto za kupata mifugo kama kuku ambao wako karibu yake au walioko tayari sehemu yoyote anayotaka, anaweza kuingia kwenye mfumo wa Agripoa na kuangalia nini anataka kununua na akapata ndani ya muda mfupi.
Wamiliki wa maduka wataweza kutumia Agripoa kutunza kumbukumbu za bidhaa zao walizo nazo. Wataweza kupata habari za uhitaji wa madawa na pembejeo toka kwa wahitaji na wataweza kuuza kwa kasi sana kupitia mtandao wa Agripoa
Kupitia Agripoa, Makampuni ya utotoleshaji wa vifaranga yataweza kupata wateja wa vifaranga kwa kuwaruhusu ku toa oda za vifaranga.
Lakini pia makampuni ya uzalishaji na usambazaji wa vyakula vya mifugo yataweza kupata wateja wake kirahisi kupitia Agripoa na kuuza bidhaa zao kirahisi sana.

Jinsi ya Kutumia Agripoa

Mfumo wa Agripoa kwa sasa unafanya kazi kwa simu za Android na unapatikana kwenye Google PlayStore. Tafadhali nenda kwenye Google PlayStore na pakua kwa kuandika "Agripoa"

Jisajiri

Jisajiri kwa kuingiza majina yako matatu pamoja na Namba ya Simu, Hii ni Rahisi Sana

Chagua nini Unapendelea

Jaza Fomu ya kuonesha nini unapendelea ili mfumo uweze kukupa vitu vyote unavyo penda.

Furahia Sasa

Sasa unaweza kuanza kufurahia kutumia App kwa bure. Utapata kila kitu ukipendacho.

Shuhuda za Wateja Wetu

Zifuatazo ni Shuhuda toka kwa Wateja wetu.

testimonials

Agripoa ni sehemu bora ya Soko langu, napata oda za wateja kabla ya siku za kuuza kufika kwa sababu kila mteja anajua ubora wa kuku wangu.

Michale Shindika - Mfugaji wa Kuku
testimonials

Agripoa inaniruhusu kutunza kumbukumbu zangu zote za ufugaji, gharama na faida. Pia naweza kutumia hizi kumbukumbu kupata mikopo.

Edner Massawe - Mfugaji wa Kuku
testimonials

Napenda sana jinsi vijana wa Agripoa, wanavyopokea simu na kutuelekeza jinsi ya kutumia mfumo wao ambao ni suluhisho kubwa.

Gration KamugishaMteja

Mawasiliano

Kuwa Huru kuwasiliana na sisi

Thank you!